Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe amemtuhumu bungeni waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Dkt Fenela Mukangara kuwa alitoa maagizo kuwa televisheni ya taifa TBC 1 ikatishe kuonesha hotuba ya mjumbe wa bunge la katiba Tundu Lissu wakati akiwasilisha maoni ya wachache kwenye bunge la katiba mwezi uliopita
Mh. Mbowe ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ambapo amesema vyombo vya habari vya umma vinatumiwa vibaya kwa kuipendelea serikali ya CCM ilihali vyombo hivyo ni mali ya umma bila kujali itikadi zao
Amesema kambi rasmi ya upinzani ilipata taarifa kuwa waziri huyo ndiye aliyewaamuru wakatishe matangazo hayo na si ubovu wa mitambo kama ilivyoelezwa hapo awali
"Nashangaa pale ambapo vyombo hivi ambavyo vinaendeshwa kwa kodi za wananchi bila kujali itikadi za vyama, au dini, sasa iweje vyombo hivi vinatumika kuipendelea serikali ya ccm tu?" amesema mbowe
Amesema anamtaka waziri mkuu Pinda kuliambia bunge ni kwa nini vyombo hivyo vya umma ambavyo ni tbc 1, tbc taifa,na magazeti ya serikali ya daily news vinatumika kwa maslahi ya serikali ya CCM tu na si kwa manufaa ya wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment