Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
TATIZO hili huwakumba watu wengi kwenye jamii lakini kwa bahati mbaya wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadaye husababisha baadhi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.
Maumivu chini ya kitovu hutokea kama ifuatavyo: Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili.
Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa urefu.

Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo maumivu ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi. Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo gani kwa wanawake?

Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huohuo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.

Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba (ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi.

Mwanamke ambaye ana maumivu chini ya kitovu na wakati huohuo ana matatizo ya hedhi, mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kuna uwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.

Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huohuo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kuna uwezekano akawa na PID hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.

Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top