Na; Hassan Hamad (OMKR).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewaongoza maelfu ya waislamu katika
mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa wa
Mwanza na mwanaharakati wa dini ya
Kiislamu marehemu sheikh Ilunga Hassan
Kapungu.
Sheikh Ilunga amefariki dunia mjini Dar es
Salaam na kuzikwa katika makaburi ya
Mwinyimkuu Magomeni.
Katika uhai wake sheikh Ilunga Kapungu
alikuwa mwanaharakati ambaye mara nyingi
alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya
dini ya Kiislamu, ambapo mwishoni mwa
mwaka 2013 alikamatwa kwa tuhuma za
uchochezi mkoani Tabora na baadaye
kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla
ya kukamatwa kwake na kuachiwa huru
Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh
Ilunga alikwenda nchini India kwa matibabu
baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo
pamoja na sukari.
Akizungumza katika mazishi hayo sheikh
Basaleh wa Dar es Salaam, amesema
marehemu sheikh Ilunga alikuwa
mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa
kuigwa katika harakati za dini ya Kiislamu.
Mazishi yake yameweka historia baada ya
maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki
kwao, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi
lake kufukiwa kwa mikono badala ya
kutumia mapauro na majembe kama
ilivyozoeleka.
Masheikh kutoka Mikoa mbali mbali ya
Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo
sheikh Kishki.Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment