Je umekuwa ukibugia mvinyo ili ili ukusaidie kiafya?
Watafiti wanadai kuwa mvinyo mwekundu (Red wine) hauna manufaa kama ilivyodhaniwa kuwa nayo kwa moyo wa binadamu.
Aidha watafiti hao wamegundua kuwa kirutubisho cha mvinyo huo ''Resveratrol'' hakizuii maradhi ya moyo wala kurefusha maisha ya wale wanayoikunywa mvinyo huo mwekundu.
Prof Richard Semba
"Hadi kufikia hapa tulipo sifa iliyolimbikiziwa kiungo cha Resveratrol eti kuwa inafaida kubwa kwa siha ya binadamu si kweli. Hakuna udhibitisho wa kisayansi unaounga mkono sifa hizo za faida kwa afya"
Utafiti huo hautakuwa wa kwanza.
Utafiti umefanywa mara nyingi nchini Ufaransa
kujaribu kutanzua kitendawili cha matukio machache sana ya maradhi ya
moyo miongoni mwa wenyeji nchini Ufaransa ikilinganishwa na mataifa
yaliyostawi ilihali asilimia kubwa ya
wafaransa ni waraibu wa vyakula vya kukaangwa kwa mafuta mengi na wanywaji wa mvinyo.
Utafiti wa awali umekuwa ukiashiria kuwa unywaji
huo wa mvinyo mwekundu ulaji wa chocolate na matunda labda ndiyo huzuia
maradhi ya moyo.Watafiti waligundua kuwa kiungo cha Resveratrol ndicho kibwagizo katika vyakula hivyo vyote na hivyo kuipigia debe kuwa ndiyo sababu ya afya nzuri ya wafaransa.
Aliwaongoza madaktari watafiti wa maradhi ya moyo kuwachunguza wakongwe 783 kutoka mji wa Tuscany ambao walitoa maelezo kuhusu siha zao vyakula wanavyokula na kunywa na hata mkojo ili kufanyiwa utafiti na kwa zaidi ya kipindi cha miaka 9.
Katika kipindi hicho cha miaka 9 wakongwe 268
walioshiriki katika utafiti huo waliaga dunia 174 walipata maradhi ya
moyo na wengine 34 walipatikana wameathirika na ugonjwa wa saratani.
Daktari wa moyo nchini Uingereza Maureen Talbot,anasema licha ya ripoti hiyo wakfu wa magonjwa ya moyo nchini Uingereza hautabadilisha ushauri wake kwa umma kuwa watu waendelee kula mboga matunda na nafaka.
>>>>bbc
<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment