- Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. PICHA|MAKTABA |
Dar es
Salaam. Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina
tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).
Taarifa
za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi
Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti
huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.
Binti
huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili
ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa
mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.
Akizungumza
na gazeti la Mwananchi nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye
alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara
mbili ndani ya gari.
Alisema
mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba
angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa
sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa
ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.
Polisi
katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini
walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na
askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi
jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana
hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati
ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake
akisema bosi wake ana kazi nyingine.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.
Mwimbaji anena
Alipoulizwa
jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani
tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana
na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.
“Of
course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa
kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused
(nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati
sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.
Kadhalika,
jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa
ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema:
“Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.
Mwananchi
lilimpigia tena simu lakini ilikatwa na baada ya hapo kila alipopigiwa
haikupokewa. Baadaye saa 6:35 mchana, mtu aliyejitambulisha kuwa ni
mdogo wa mtuhumiwa alipiga simu chumba cha habari akitaka kuonana na
mhariri wa gazeti hili, kwa maelezo kwamba alipewa namba husika na kaka
yake.
“Samahani,
mimi (anataja ina) niko hapa nje Ofisi za Mwananchi, nilifika hapa
kutaka kuonana na mhariri maana nasikia mwandishi wenu alikuwepo polisi
tangu jana kwenye tatizo lililompata kaka yangu, sasa wakati nasubiri
kuonana na mhariri kaka amenipigia simu akisema namba hii imempigia, kwa
hiyo naomba tuonane ili tuzungumze tuone jinsi ya kumsaidia,” alisema.
Baada ya
kuonana na mwandishi wa habari wa gazeti hili, alisema suala hilo
lilikuwa likijadiliwa katika ngazi ya familia, hivyo wasingependa
liandikwe kwenye vyombo vya habari.
Vipimo vya hospitali
Juzi,
baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali
ya Amana ambako alifunguliwa faili la matibabu na kupewa namba ya
usajili 667. Aliingia chumba cha matibabu namba 21 kumuona daktari kwa
ajili ya vipimo zaidi.
Matokeo
ya vipimo yalionyesha kuwa binti huyo alikuwa amefanya ngono kwa nguvu.
Katika fomu hiyo ya uchunguzi, daktari aliandika ‘High vagina swab’.
Baada ya
vipimo, familia ilirudi katika Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya
vipimo vya daktari, hivyo kufungua faili la kesi lililopewa namba RB
TBT/RB/319/2014 na namba TBT/IR/1865/2014. Jana binti huyo alikwenda
tena Amana ambako alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU na mimba. Vipimo
vya awali vya VVU vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika na hakupata
ujauzito.
Mtoto alipo
Habari
ambazo zililifikia gazeti la Mwananchi jana jioni, zilisema mtoto
aliyebakwa alichukuliwa na familia ya Mchungaji Josephat Gwajima.
Mwananchi
lilifanya jitihada za kumtafuta Mchungaji Gwajima bila mafanikio,
lakini lilimpata mkewe, Grace ambaye hakuwa tayari kuthibitisha kuwapo
au kutokuwapo kwa mtoto huyo nyumbani kwake.
“Naomba
nisiwe msemaji katika jambo hilo, yupo msemaji mwenyewe ambaye naamini
mnamfahamu naye ni Mchungaji Gwajima, kwa hiyo mtafuteni, yeye atasema
kama mtoto yupo hapa au hayupo na kama yupo sababu zake ni zipi,”
alisema Grace.
Alipoombwa
atoe mawasiliano ya simu ya mchungaji huyo, Grace alisema: “Kwa kweli
kama unaweza, kesho nenda pale Kanisani Kawe utapewa utaratibu wa
kuonana naye.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment