Katika
ulimwengu wa leo neno blog siyo kitu kigeni, leo hii karibu kila
mtumiaji wa internet anayo blog yake. Blogu hizi kuna zile
zinazotembelewa na watu wengi na kuna zile zinazopata watembeleaji kwa mdondo.
Je umewahi kujiuliza kwanini watu hawatembelei blog yako kama wanavofanya kwa blog fulanifulani? Ingawa kuna sababu nyingi kama
umri wa blog, umarufu wa mmiliki wa blog nk lakini kuna kuna vitu
ambavyo unaweza kuvifanya na vikakuongezea idadi ya watembeleaji.
Hivyo kwenye makala ya leo tutaangalia ni vitu gani vya msingi kuzingatia ili blog yako ivutie wasomaji wengi zaidi.
1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.
Kama
umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi
zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na
hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule.
Ingawa
ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi
(blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi,
ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.
Siyo
tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao
hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.
Hivyo,
jambo la muhimu ni kuchagua uelekeo unaoupenda na kuuweza, mara nyingi
kazi ya kublog huwa rahisi kama unablogu kitu unachokipenda, mfano,
binafsi nikiwa ninaandika makala zenye uelekeo wa IT kwenye Blog ya PamojaLink,
kwakuwa ninapenda IT na ndiyo maisha yangu ya kila siku hivyo kwangu
kuandika makala za IT ni sehemu ya maisha yangu, na jinsi kazi
inavyokuwa rahisi ndivyo utakavyoweza kuandika makala nyingi zaidi na
zenye mvuto zaidi, hivyo huvutia wengi zaidi.
Pia
jinsi unavyokuwa wa kipekee, ndivyo unavyopata watemebeleaji wengi
zaidi, mfano, badala ya kukimbilia kwenye blogu za habari na michapo,
kwanini usijikite kwenye blogu za yanayoendelea vyuoni na kuonesha
maisha ya wanafunzi, kwanini isiwe blogu ya hadha ya usafiri na foleni
nk.
Wana
blogu wanatakiwa kuwa wabunifu, wawe watu wanaofikisha maono yao juu ya
mambo ya kijamii kwa kutumia intaneti, na wao ndiyo wataisaidia jamii
yetu.
Kumbuka; Unapochagua
uelekeo,itakusaidia kujua nani mlengwa wako, na vitu gani muhimu huyo
mlengwa wako vinamuhusisha, hapa utaangalia mambo kama elimu, upeo wa
uelewaji na hata vitu wanavyopenda kusoma. Kwa kujua vitu hivi
itakusaidia kuandika makala zinazosomwa na zenye kueleweka na wahusika.
Kumbuka, haublogu ili usome wewe mwenyewe bali ni kwa ajili ya
watemebeleaji wako. Hivyo kuwafahamu wao ni moja ya hatua muhimu
itakayowawezesha kusoma na kuzipenda makala zako.
2. Tumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ni kitu cha lazima kama unataka kuongeza watemebeleaji wa blogu yako.Mitandao
hii ni vijiwe vya mamilioni ya watemebeleaji ambao pia ni watemebeleaji
wa blogu yako pia, hivyo ni lazima uhakikishe unatumia vyema mitandao
hii.
Hakikisha
kila makala ya blogu yako inaenda moja kwa moja kwenye mitandao jamii,
pia hakikisha kwenye kila makala kuna kitufe cha share, like, g+ nk
mbavyo vitawawezesha muingiliano na mitandao jamii.
Ingawa
mitandao jamii ni muhimu, lakini, epuka matumizi yaliyozidi na hata
kuwachukiza watembeleaji, kuna baadhi ya blogu kila unapofungua
unakutana na kidirisha cha
kulike
ambacho hukuzuia kufanya lolote mpaka ulike kurasa ya Facebook. Hi
inaweza kuwa kero kwa watembeleaji wa blogu yako. Kitu cha muhimu hapa
ni, usiwalazimishe
watu kulike au kushare makala zako, bali washawishi kwa ubora wa makala.
3. Blogu yako iwe na spidi ya haraka
Je
ni watu wangapi wapo tayari kusubiria dakika tano mpaka blogu yako
ikawa tayari kufunguka? Kama wewe blogu yako ni mpya, ni dhahiri kuwa
hakuna atakayesubiri, na kama wewe blogu yako ni maarufu, basi
watasubiri kwakuwa hakuna mbadala na pindi watakapopata mbadala basi
wataanza kupungua siku hadi siku.
Blogu
kuchelewa kufunguka kunaweza kusababishwa na mambo mnegi kama uwingi wa
makala, teknolojia iliyotumika na hata mrundikano wa vitu; mfano,
kwenye blogu nyingi za Tanzania, kumekuwa na rundo la matangazo kabla ya
kuanza kwa makala, na matangazo haya ni picha kubwa ambazo kila moja
inachukua ujazo tosha na kuifanya blogu iwe taratibu sana.
Kuna
njia nyingi za kuonesha makala na matangazo idadi sawa kwa mtindo ambao
hautoathiri spidi ya blogu yako ambayo nimeielezea kwenye kipengele cha
muonekano.
4. Fikiria jina kamili
Blogu kama ilivyo Website, inaweza kuwa na jina, leo hii kuna blogu nyingi sana maarufu zina majina, kama www.pamojalink.com, www.bongoswaggz.com nk,
kuwa na jina kamili la blog yako kutasaidia kukumbukika na pia
itakusaidia kwenye mitandao ya utafutaji. Si hayo tu, pia itakusaidia
pindi unapotaka kuhamia kwenye website kamili kwani hautatakiwa
kuwataarifu watembeleaji tena.
Nimewahi kuandika mambo ya kuzingatia pindi uchaguapo majina ya website / blog
Kwa
wale wanaotumia Blogspot, unaweza kununua jina (domain) halafu
ukalielekeza kwenye blogspot na watu wakatumia jina kamili kufungua blog
yako na sio .blogspot.com tena ila wewe utaendelea kuichunga kwenye
blogspot kama kawaida.
Gharama ya jina haizidi elfu 20 ya kitanzania, unaweza nunua kwa kwenda hapa
5. Muonekano bora ni kitu cha lazima
Kwenye
falsafa ya watumiaji wa mitandao tunasema; mtembeleaji wa wavuti
hutumia sekunde zisizozidi tatu kutafuta anachokitaka na kama atashindwa
kukipata, basi kutimka, hivyo blogu yako ni lazima iwe na uwezo wa
kufikisha ujumbe na kumvutia somaji ndani ya sekunde tatu.
Blogu
isiyovutia haiwezi kuwa na watembeleaji wengi, na hata kama wengi
wanakuja, basi hutimka (baunce) bila kusoma chochote. Leo hii kuna
makampuni mengi sana yanayoweza kukusaidia kutengeneza blogu au website
kwa gharama nafuu kabisa, unaweza kutafuta kwa kuandika website design in tanzania kwenye google na kuangalia makampuni yanayoweza kukusaidia.
Ingawa
mitandao ya blog kama Bloggers ni mizuri kwa kuanzia, ila jinsi blog
yako inavyozidi kukua, ndivyo umuhimu wa kuwa na blog inayojitegema
unavyoongezeka.
Gharama za kutengeneza blog isiyo ya blogspot.com si ghali na hi itakupa uwanja mpana wa kuchunga na kuiboresha blog yako.
6. Takwimu ni muhimu pia
Ingawa
mada ni jinsi ya kuongeza wasomaji wa blog yako, lakini hatuwezi kuacha
kuongelea umuhimu wa takwimu. Kuna usemi unaosema, kama usipoipima,
basi hautoweza kuiboresha. Hivyo kwa kuwa na takwimu ya watembeleaji wa
blog yako, siyo tu itakuwezesha kujua mtiririko wa wasomaji, bali
wanapotoka, wanatumia muda gani kwenye blog yako nk.
Takwimu
zitakusaidia kupanga mikakati ya kujitanua na kujitangaza zaidi, pia
zitakuwezesha kuthaminisha harakati zako za ukuaji. Na takwimu hizi
zinapatikana kwa kwenda Google Analytics.
7. Usisahau watumiaji wa simu
Takwimu
zinaonesha, watumiaji wa intanet wengi hutumia simu za mkononi
kufungulia website, na idadi hii huongezeka siku hadi siku. Hivyo, kama
wewe ni mmiliki wa Blog, hakikisha blog yako inaonekana vyema kwa watumiaji wa simu.
Kama
website yako haifunguki kwenye simu, basi jua kwamba unapoteza mamia ya
watembeleaji siku hadi siku. Hivyo wakati ndiyo huu, nenda kisimusimu
zaidi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment