KASHFA kubwa idara ya mahakama Iringa ni baada ya hakimu mmoja
wa mahakama mjini hapa kufumaniwa ndani ya gari ya mwanamke ambae ni
mke wa mpiga picha mmoja maarufu mjini hapa akivunja amri ya sita
ndani ya gari nje ya ofisi ya mahakama ya Mwanzo bomani na jirani na
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa.
Tukio hilo
la aibu limetokea usiku wa jana ambapo hakimu huyo ambae anadaiwa
kuongoza kwa michepuko na wake za watu alifumwa na njemba lenye mke
akiendelea kufungua kurasa za mama huyo ambae pia ni mwalimu wa shule
moja za kimataifa katika barabara ya Iringa-Dodoma
Mwandishi wetu alielezwa kuwa mpiga
picha huyo maarufu mjini hapa kwa muda amekuwa na mgogoro wa ndoa na
mkewe huyo kutokana na mwanamke kuendekeza michepuko na wanaume
tofauti tofauti akiwemo hata paroko .
Kutokana na hali hiyo jembe hilo
liliamua kufikisha suala hilo mbele ya pirato kwa kutoka ndoa hiyo
ivunjjike na mahakama hiyo ya mwanzo inadaiwa kuhukumu kimagumashi na
hivyo jemba hilo kuamua kusonga mbele zaidi na kesi hiyo kuwa
mikononi mwa hakimu huyo aliyefumwa akivunja amri ya sita ndani ya
gari.
Hakimu huyo ambae jina lake linaanzia
na herufi A baada ya kufumaniwa alilazimika kuendesha gari hilo kwa
mwendo kasi kukwepa kichapo huku wakiwa hawajajisitili vema kutokana na
nguo zao kuvua ,kabla ya jemba lenye mke kufukuza kwa boda boda na
kuungwa mkono na waendesha boda boda ambao walifanikiwa kumkamata
hakimu huyo na mama mke wa mtu na kuwapa kichapo kiasi cha hakimu
huyo.
Hata hivyo mbali ya kukutwa na mke wa
mtu hakimu huyo alikimbilia polisi kufungua kesi ya kimagumashi
kuwa eti ameibiwa pesa shilingili laki mbili .
>>>>Chanzo www.francisgodwin
<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment