DEREVA
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Juma Juma (52)
amefariki dunia wakati akifanya mapenzi na mwanamke mhudumu wa baa
kwenye nyumba ya kulala wageni.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea mei tatu mwaka huu saa nane za usiku chumba no.S.2 nyumba
ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New Kiomboi mjini.
Kamanda
huyo amesema siku ya tukio kuwa dereva Juma aliondoka nyumbani kwake
mida ya saa sita za usiku alimwaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja
na hatachelewa kurudi nyumbani kwa hiyo alifunga mlango wa mbele ya
nyumba.
Amesema
kuwa masaa mawili baadaye Juma alionekana akiwa baa iliyoko kwenye
nyumba hiyo la kulala wageni iliyoko umbali wa mita 50 kutoka nyumbani
kwake.
“Muda
huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo alitwaye
Agness Mayo (32) anayesadikika kuwa na uhusinao wa kimapenzi na Juma.”
Kamwela
amesema mhudumu huyo wa baa mpenzi wa Juma, alitoweka mei nne mwaka huu
baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.
Hata hivyo, ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wa baa.
Kamanda
huyo amesema kuwa toka siku hiyo ya mei tatu chumba alicholala Juma
hakikufunguliwa hadi mei tano mwaka huu na ndipo mwili wa dereva huyo
ulipokutwa ukiwa umeharibika vibaya.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment