MWIGIZAJI wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo’ amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Kiwalani jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo makini, Gabo aliyekuwa katika gari binafsi, aligongana na gari lingine na kupata jeraha mguuni hivyo kulazimika kulazwa kwa takriban wiki tatu kisha kuruhisiwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na paparazi wetu baada ya
kutoka hospitali, Gabo aliyeitendea haki Sinema ya Majanga ya Mahsein
Awadh ‘Dk Cheni’, alieleza mazingira ya ajali.
“Nilikuwa naendeshwa na rafiki yangu
lakini ghafla tukagongana uso kwa uso na gari lingine, nashukuru magari
hayakuumia sana lakini mimi nililazwa kwa wiki tatu kutokana na jeraha
nililolipata mguuni,” alisema Gabo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment