Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Solange alimshambulia Jay Z katika lift walipokuwa wanatoka tamashani
Mfanyakazi aliyefichua kanda inayoonyesha mwanamuziki Jay Z akishambuliwa na shemeji yake , amefutwa kazi.
Kamera ya lifti ilinasa vurumai kati ya Jay Z na shemeji yake Solange Knowles aliyeonekana kuwa na hasira mno huku akimshambulia Jay Z , ingawa haijulikani kilichosababisha vita hivyo kwenye lifti.
Kanda hiyo ya video ambayo ilitolewa kwanza kwenye tovuti ya udaku kuhusu watu maarufu TMZ, ilimwonyesha dadake Beyonce akimpiga Jay Z baada ya tamsha la Met mjini Los Angeles, iliyofanyika mwezi Mei tarehe 5.

Baada ya ugomvi mkali baina yao, mlinzi aliingilia kati. Hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti.
Hoteli hiyo inayojulikana kama ‘The Standard ilisema kuwa ilishtushwa sana na kufichuliwa kwa matukio ya Lifti na ikamtaja mfanyakazi huyo aliyehusika katika ufichuzi huo.

Mfanyikazi huyo alifutwa kazi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama kwa kufichua video za CCTV, ambazo ni za siri.
Hoteli hiyo iliongeza kuwa ingetoa habari zingine zote za ziada kwa idara ya kupambana na wakiukaji wa sheria.
Waakilishi wa Jay Z, Beyonce na Solange hawajasema lolote kuhusiana na tukio hilo.
<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>> 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top