Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya. Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne. Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment