Morogoro.
Hali ya mtoto Nasra Rashid (4) aliyekuwa amefichwa kwenye boksi kwa
miaka minne, imebadilika ghafla juzi na jana kuwalazimu madaktari
kumweka katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.(Martha
Magessa)
Mganga
Mkuu Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema jana kuwa
tatizo kubwa la mtoto huyo ni kubadilika ghafla kwa upumuaji wake na
utaratibu unafanyika ili leo asafirishwe kupelekwa Dar es Salaam kwa
matibabu zaidi.
"Tunatarajia kumpeleka Muhimbili mapema asubuhi kwa gari maalumu la wagonjwa ili kupata matibabu zaidi," alisema Dk Lyamuya.
Alisema juzi Nasra alikuwa mwenye furaha na mchangamfu lakini jioni yake hali ilibadilika katika mfumo wake wa kupumua.
Alisema
kwa msingi huo, uongozi wa hospitali ya mkoa umeamua kumsafirisha kwenda
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya
yake.
Uchunguzi
wa awali wa afya ya Nasra ulibaini kuwa mtoto huyo alikuwa na maradhi
ya nimonia (kichomi), mifupa ya miguu na mikono kuvunjika pamoja na
utapiamlo.
Watuhumiwa kortini
Katika
hatua nyingine, watu watatu akiwamo baba mzazi wa Nasra, wamefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kujibu mashtaka ya kula njama
na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.
Baba wa
mtoto huyo Rashid Mvungi (47), mama mlezi wa Nasra, Mariamu Said (38) na
mumewe Mtonga Omar (30), walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mary Moyo jana na kusomewa mashtaka hayo.
Wakili wa
Serikali, Sunday Hyera alidai kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo
kati ya Desemba, 2010 na Mei mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege,
mjini Morogoro.
Alidai
kuwa katika kipindi hicho walimfanyia ukatili wa kumtelekeza na kumpa
malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa.
Alitaja maradhi yaliyomkumba akiwa ndani ya boksi ni utapiamlo, kichomi na mvunjiko wa mifupa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment