Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HATIMAYE safari ya mechi 26 za ligi kuu
soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014
imemalizika leo kwa timu zote 14 kushuka
uwanjani katika miji tofauti nchini.
Yanga waliovuliwa ubingwa na Azam fc
walikuwa wenyeji wa watani zao wa jadi,
wekundu wa Msimbazi Simba sc kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mechi hii ya kulinda heshima kwa timu zote
ilianza kwa timu zote kucheza kwa umakini,
lakini Simba walionekana kutawala mchezo
huo na kufanya mashambulizi mengi langoni
mwa Yanga.
Katika kipindi hicho cha kwanza, Amiss
Tambwe, Said Ndemla kwa nyakati tofauti
walipata nafasi nzuri za kufunga lakini
kukosa umakini kuliwanyima Simba mabao.
Yanga nao walifika mara kadhaa langoni
mwa Simba, lakini Mrisho Ngassa na Didier
Kavumbagu walishindwa kuzibadili nafasi
hizo kuwa mabao.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza kilikuwa
katika himaya ya Simba kwasababu walifika
mara nyingi zaidi langoni mwa Yanga na
pengine katika mechi za nyuma wangekuwa
wanacheza mpira kama ule wasingekuwa
hapo walipo.
Kipindi cha kwanza kilimazika kwa timu hizo
kutofungana.
Kipindi cha pili, Yanga walitawala zaidi
mchezo, lakini dakika 75 Haruna Chanongo
aliifungia Simba bao la kuongoza.
Dakika ya 86 ya kipindi hicho, Saimon Msuva
alichomoa bao hilo na mechi kumalizika kwa
sare ya 1-1.
Hata hivyo katika mchezo huo kulitokea
vituko kadhaa.
Cha kwanza ni mshambuliaji wa Yanga Didier
Kavumbagu kutoa taulo la mlinda mlango wa
Simba Ivo Mapunda alilolitundika kwenye
nyavu golini.
Kitendo hicho kinatafsiriwa kuwa ni imani
za kishirikina kwa wachezaji wa Yanga
walioamii taulo hilo limezuia mabao.
Kutokana na purukushani hiyo, mwamuzi wa
mchezo huo alimzawadia kadi ya njano
Kavumbagu na Ivo akapewa taulo lingine.
Dakika chache baadaye, shabiki mmoja
aliingia uwanjani na kuiba taulo la Ivo na
kulirusha kwa mashabiki wa Yanga, lakini
alitiwa mbaroni na Polisi walioshindwa
kumuona wakati anaingia.
Hata hivyo baada ya Simba kufunga bao,
dakika chache baadaye, kocha msaidizi wa
Simba, Suleiman Matola na kocha wa makipa
Idd Pazzi walitolewa ka kadi nyekundu.
Kwa matokeo ya mechi zote endelea
kutufuatilia na muda si mrefu utapata
pamoja na uchambuzi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top