Mama Shakila Bakari (30), mkazi wa Mbagala jijini Dar.
Mwanamke
mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala
jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina
linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili
aliojifungua Machi 28, mwaka huu.Akizungumza na gazeti hili juzi,
Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto
wake wa kwanza,lakini kukatokea hitilafu ndogo ya mwanaye huyo kukatwa
kidogo na mkasi uliosababisha jeraha kwenye paji la uso.
“Waliniambia
walimgusa kidogo kwa bahati mbaya na mkasi, lakini wakasema hakuna
tatizo, waliniwekea kifuani na damu ikawa imenivujia kidogo, baadaye
nilijisikia uchungu tena, manesi wakamtoa mtoto yule kifuani kwangu ili
nipate nafasi ya kujifungua tena, nilipojifungua walinionyesha motto wa
kiume,” alidai mama huyo.
Shakila
alidai kuwa, tofauti na matarajio yake, alikabidhiwa mtoto
aliyejifungua wakati huo huku Yule wa mwanzo akipewa maelezo
yasiyoeleweka. “Niliwashangaa manesi. Waliponiona sibabaiki kuhusiana na
mtoto wangu ndipo wakaniletea mtoto mwingine wakidai kuwa ndiye huyo.
Nilipomchunguza nilibaini kuwa alikuwa wa kiume wakati mimi nilimzaa wa
kike, halafu huyu niliyeletewa hakuwa na kijereha.
”Baada
ya kumkataa mtoto huyo, Shakila alidai manesi waliondoka na kichanga
kile na katika hali ya kushangaza, walisimamia kauli yao ya awali kuwa
hakuzaa motto mwingine zaidi ya huyo aliyekuwa naye.
Dada
wa Shakila aliyejitambulisha kwa jina la Sikujua Bakari alisemawakati
mdogo wake akijifungua yeye pamoja na shemeji yake (mume wa Shakila)
hawakuruhusiwa kuingia ndani, lakini baada ya kujifungua walikwenda
kumuona akiwa na mtoto mmoja wa kiume, walipompa pongezi walipatwa na
mshangao.
chanzo>>>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment