Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa
Bunge la Katiba Kutoka Chama cha
Demokrasia na Maendeleo,Cuf na
NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa
UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba
kwa Madai wamechoka Kutukana na
Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu
Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa
Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014
hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha
kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta
Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa
Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu
ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba
ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za
Malipo ya Posho na seating allowance
zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014
ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za
Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka
tar.20/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa
hizo,Mwandishi wetu alizungumza na
Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo
unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe
(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote
zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha
siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba
zao za Benki na Malipo yote hupitia
huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.
Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema
wanaojiita UKAWA toka jana walijua
wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia
kwenye account zao Binafsi. Mambo
yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa
Fedha(Sera) Mh:Mwigulu kuagiza leo form
zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22
mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na
asile.
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na
clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe
wakiojitoa na badala yake awateue watu
waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko
hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga
njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu
alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa
Wazabuni wanaozidai halmshauri,
wangeweza kulipa madeni ya walimu, au
kuwapa mikopo watoto wa masikini
waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa
mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini,
au zingepeleka umeme, maji, vitabu au
barabara lakini wamelipwa wajumbe badala
ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya
kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta
visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea
Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za
Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25
mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu waziri wa fedha MH NCHEMBA.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top