Na Rose Chapewa, Mbeya
Mwanafunzin Sabrina Athuman (11) anayesoma darasa la nne skuli ya msingi Kagera
jijini Mbeya, ametoweka nyumbani kwao
tokea Aprili 26 mwaka huu katika
mazingira ya kutatanisha.
Baba mlezi wa mtoto huyo, Jumbe Said Zungiza,
akizungumza na gazeti hili alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwao eneo la
mama John kata ya Ilomba jijini hapa Aprili 26 mwaka huu majira ya saa 1:00
asubuhi bila kuaga.
“Kawaida huwa tunajua kuwa mtoto wetu siku za Jumamosi
huwa anaenda skuli kwenye mitihani na
kabla hajaenda kawaida huwa tunampa shilingi 500 ya mtihani lakini cha
kushangaza siku hiyo tulishtuka kuona hayupo na kitendo cha kutoaga kilituchanganya
ikabidi tuingie chumbani kwake lakini hatukufanikiwa kumuona mpaka sasa,”alisema.
Akizungumzia kuhusu mazingira ya kupotea kwa mtoto
huyo, alisema mazingira aliyoondoka mtoto huyo yanazidi kuwapa wasiwasi kwani
aliondoka asubuhi sana
na kilichowafanya wazazi hao kushtuka ni baada ya kuamka kuona milango ya nje
ipo wazi ndipo walipoanza kuita lakini hakuitika.
Kwa upande wake mama mlezi wa mtoto huyo, Riziki
Jumbe, alisema Aprili 26 mwaka siku alipotoweka mtoto huyo nyumbani alikuwa amevaa
suruali yenye rangi mchanganyiko ambayo ni nyekundu,kijani, bluu, pamoja hijabu
nyeupe kichwani.
Aidha alisema rangi ya mtoto huyo ni maji ya
kunde, mrefu mwemba na kwamba mara nyingi anapenda kutembelea maeneo ya Mswiswi kwa mjomba wake lakini huko hajaonekana.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment