Marehemu Majaliwa akiwa hoi hospitalini kabla ya kufariki dunia
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa Majaliwa alifariki dunia
muda mchache badae wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo kutokana
na kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake. Hata hivyo mmiliki wa
Nyumba iliyobomolewa madirisha hayo bado hajajulikana kutokana na kuwa
bado inaendelea kujengwa.
Madirisha yanayodaiwa kuibwa na Majaliwa.
Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na linaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Majaliwa mkazi wa
Majengo mjini Kahama mkoani Shinyanga ambaye ni fundi nyumba amefariki
dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama
baada ya kupigwa na kisha kuchomwa moto na wananchi kwa tuhuma za kuiba
madirisha ya nondo.
Amesema wanachi walianza kumfuatilia na walipomkamata alianza kukimbia
ndipo wananchi hao wakapiga kelele na kusababisha kumkamata na kuanza
kumrushia mawe kisha kumchoma moto kwa mafuta ya Petroli ambayo
yalipatikana katika pikipiki.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven tukio hilo
limetokea leo majira ya saa 11 alfajiri ambapo mtuhumiwa alivunja
madirisha hayo katika nyumba inayoendelea kujengwa na baadhi ya watu
kumuona.
Mseveni amesema mtuhumiwa huyo alijirusha kwenye mtaro wa maji na moto
huo ukazima na kwamba ilipigwa simu kwa jeshi la polisi ambao walifika
eneo la tukio na kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Akiongea kwa shida katika hospitali ya hiyo kabla ya kifo chake
mtuhumiwa huyo alisema alipigiwa simu na dada mmoja aliyemtaja kwa jina
moja la Manka kwamba afuate mzigo huo ili ampelekee na ghafla wananchi
walimzingira na kuanza kumpiga na kumchoma moto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa Majaliwa alifariki
dunia muda mchache badae wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo
kutokana na kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
Hata hivyo mmiliki wa Nyumba iliyobomolewa madirisha hayo bado hajajulikana kutokana na kuwa bado inaendelea kujengwa.
Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na linaendelea na uchunguzi zaidi.
>>>>>www.farajimfinanga.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment