
MJohn Terry, David Luiz, Petr Cech na Cesar Azpilicueta wakiduwaa baada ya kujifunga bao la pili

Luiz hakuweza kuuzuia mpira usizame nyavuni

Kufungwa kubaya, cheki Luiz anavyoshangaa baada ya kuwafungia PSG bao la pili

Faida kwa PSG: Pastore akizingirwa na wenzake baada ya kufunga bao la tatu
Hakuna furaha tena: Jose Mourinho akifoka

Kapelekwa sokoni: Hazard akimpoteza kipa wa PSG , Salvatore Sirigu na kuandika bao la kusawazisha kwa penati pekee waliyopata

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao lao
Katika
mechi nyingine iliyochezwa usiku huu, Real Madrid waliwaalika Borussia
Dortmund katika uwanja wa Santiago, Bernabeu na kushuhudia wajerumani
hao wakipigwa mabao 3-0.
Mwanasoka
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameifikia rekodi ya mabao ya hasimu
wake Lionel Messi wa Barcelona katika ligi ya mabingwa barani Ulaya
baada ya kufunga bao lake la 14 usiku huu , hivyo kuifikia rekodi hiyo
ya mabao 14 ya Messi katika msimu mmoja wa UEFA.
Ronaldo
ambaye hakuwa katika kiwango chake alifunga bao la tatu katika ushindi
wa leo, lakini alitoka uwanjani baada ya kupata majeruhi na kuwafanya
mashabiki wote wa Real Madrid kusimama na kumpigia makofi wakati
anakwenda benchi.
Katika
mechi yake ya 100 ya ligi ya mabingwa, Ronaldo amefikisha mabao 49
aliyowahi kufunga Alfredo Di Stefano katika michuano ya Ulaya.
Pia Ronaldo katika mchezo wa leo alimsaidi Gareth Bale kufunga bao la kwanza.
Kikosi
cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio
Coentrao, Modric, Alonso, Isco (Illarramendi 71), Bale, Benzema (Morata
75), Ronaldo (Casemiro 80).
Mabao yamefungwa na: Bale 3, Isco 27, Ronaldo 57.
Kikosi
cha Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek (Schieber 67), Hummels,
Papastathopoulos, Durm, Kehl (Jojic 74), Sahin, Grosskreutz, Mkhitaryan
(Hofmann 64), Reus, Aubameyang.

Kazi nzuri: Gareth Bale akifunga bao la kuongoza kwa Real Madrid

Jembe: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 14 katika msimu mmoja wa UEFA

Anaunguruma: Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake
BEKI wa Chelsea, David Luiz amejifunga bao na kuwanufaisha zaidi Paris Saint-Germain katika ushindi wa nyumbani wa mabao 3-1 usiku huu katika mechi ya kwanza ya robo fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Lavezzi
alianza kufunga karamu ya mabao kwa PSG katika dakika ya 4 ya kipindi
cha kwanza. Dakika ya 27, Hazard aliisawazishia Chelsea bao hilo kwa
njia ya mkwaju wa penati na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi
cha pili, nyota ya mabingwa wa Ufaransa iliendelea kung`ara ambapo
dakika ya 62, David Luiz alijifunga na kuufanya ubao wa matokeo usomeke
2-1.
Wakati Chelsea wakihaha kutaka kusawazisha bao hilo, dakika ya 90 ya mchezo, Javier Pastore aliandika baoa la tatu na kuwanyamazisha ghafla mashabiki wa wazee wa darajani.
Baada
ya kumalizika kwa mechi hiyo, Kocha wa Chelsea alisalimiana isivyokuwa
kawaida yake na benchi la ufundi la PSG, lakini haijajulikana kama
amewakubali sana au vipi.
Zilisalia
dakika 28 pekee kwa Chelsea kutoa sare, lakini bao la kujifunga la Luiz
liliwachanganya na kubadili upepo wa mchezo. Na kabla ya hapo walikuwa
wamejiamini kufanya vizuri.
Kikosi
cha PSG: Sirigu 6, Jallet 6.5, Alex 6.5, Thiago Silva 6, Maxwell 6.5,
Verratti 6 (Cabaye 76), Thiago Motta 6.5, Matuidi 6.5, Cavani 7,
Ibrahimovic 6 (Lucas Moura 68), Lavezzi 8 (Pastore 84).
Kikosi
cha Chelsea: Cech 5.5, Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6,
Ramires 6, Luiz 6.5, Willian 6.5, Oscar 6 (Lampard 72), Hazard 7,
Schurrle 5 (Torres 59)
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment