Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Askari Polisi Kitengo cha usalama barabarani wakiuchukua mwili wa mtoto aliyegongwa na basi la kampuni ya A.M maeneo ya Ipuli Mnadani ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza,katika ajali hiyo watu kadhaa wamejeruhiwa.
Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya
Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.
Wananchi wakishuhudia mwili wa mtoto aliyegongwa na basi hilo ambapo walishauri Serikali iliifungie kampuni hiyo ya A.M kuleta mabasi mkoani Tabora ambayo walidai kuwa ni mabovu na yanausalama mdogo kwa wasafiri.
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika  kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu



 Na Mwandishi wetu Tabora.
Kufuatia kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama kwa wasafiri na wapita njia.

Wananchi hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.


Aidha wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa wa Tabora.


Wameitahadharisha Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima. 

<<<<BOFYA HAPA>>>> 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top