
Jamaa kama 30 wa abiria wa
Uchina waliotoweka na ndege ya Malaysia wamesafiri hadi Kualu Lumpur,
mji mkuu wa Malaysia, kuwahimiza wakuu wajibu maswali yao.
Wanataka wakuu wa Malaysia waombe msamaha kwa kusema kuwa ndege hiyo imepotea katika Bahari Hindi na kwa kuchelewa kutoa habari hizo.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa kuwasili kwao kulizua hali ya wasiwasi na familia hizo zilipewa ulinzi mkali na watu wa Malaysia waliojitolea, na hivyo kuwa vigumu kwa waandishi wa habari kuwafikia.
Na bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment