Inasemekana Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na Jacqueline Patrick ndiyo wanaoongoza kwa kugombewa na wanaume, wakitaka kuigiza nao kwenye filamu au video kwani siyo ‘wachoyo’ wa kujiachia wakati wa kurekodi.

Kwa mujibu wa madairekta, maprodyuza na waigizaji wakubwa wa filamu waliozungumza na gazeti hili juu ya ishu hiyo, ukipata bahati ya kufanya nao vipande vya mapenzi utafaidi kwani si wabishi wa kutoa ushirikiano.

Huku ikitolewa mifano kadha wa kadha, Uwoya alishuhudiwa kwenye filamu alizocheza na Jacob Steven ‘JB’ huku Aunt na Jack Patrick wakiibuka kidedea kwa kujiachia kihasara kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment