Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose Ndauka,ambaye waliachana tangu 2006.
 
Akizungumza na XXL ya Clouds Fm leo Tunda amesema walikuwa wakikutana na mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea kuanza mahusiano yao yamapenzi.
Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla, hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae, nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top