Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Stori: Shani Ramadhani
STAA wa kitambo kwenye filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amenaswa akipiga mitungi kwa sana ikiwa ni sehemu ya kufurahia uongozi mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity.

Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar ambapo uchaguzi wa safu mpya ya uongozi wa klabu hiyo ulimalizika na matokeo kuwatangaza mwenyekiti mpya Steven Mengele ‘Nyerere’ na wenzake kuwa washindi.

Katika mahojiano na mwandishi wetu, Johari alisema: “Kwa upande wangu ninawaamini viongozi wote waliochaguliwa katika kutuletea maendeleo katika klabu yetu kwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano. Wote nawaamini na kusema kweli, hawa ndiyo viongozi tuliokuwa tunawataka.”

Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Katibu Mkuu Willium Mtitu, Katibu Msaidizi Devotha Mbaga, Mweka Hazina Issa Mussa ‘Cloud’ na msaidizi wake Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Source:Global Publishers

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top