Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mh. Cathy Magige

Mheshimiwa Cathy Magige, amewataka wale wote wanamuhusisha kuwa na video yake akiwa Zitto Dubai kuitoa kwa public au popote inapoweza kuonekana na Wananchi ili ukweli uonekane wazi kuliko wanachokifanya sasa hivi yaani kumchafulia jina bila sababu. Mheshimiwa Cathy, Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM aliyasema hayo leo kwa simu akiongea na Blog ya mwananchi amesshitushwa sana na ujumbe wa simu ambao umekuwa ukisambazwa kila kona ya Tanzania na hata kumfikia Dada yake aliyeko Ohio, ambaye alimtumia mara moja baada ya kupokea tu ujumbe huo. Pamoja na maelezo mengi sana yakumtukana Zitto ujumbe huo unasomeka hivi:-

"Hii email itapokewa na zaidi ya watu 50. Nimeifanya makusudi, na kama unabisha haukwenda Dubai na Catherine Magige, niko tayari kuweka scanned copies ticket zenu na video zenu za siri mkiwa huko"


Mheshimiwa Magige, anawaomba wale wanaohusika na kusambaza ujumbe huu mitandaoni na kwenye simu za watu wajitokeze na kutoa ushahidi huo wa Video na copy za Ticket walizosafiria kama ni kweli wanazo ama sivyo waache uzushi huo ambao anasema hauna maana na wala hauna ukweli wowote. Mheshimiwa anasisistiza kwamba tatizo lao ni Zitto sasa haelewi ni kwa nini wanajaribu kuchafua na wengine wasio na makosa kama yeye, 

anarudia tena kwa wale wote wanaodai kuwa na huo ushahidi wa yeye kuwa na Zitto, popote pale watoe ushahidi huo ili ukweli uonekane wazi na wananchi wote badala ya uzushi usio na maana wenye nia ya kumchafulia jina.   
source blog ya wananchi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top