Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG-20140126-WA0003
IMG-20140126-WA0006
 Malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kucharangwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
Mbali na malori kuna Mabasi ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambao wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au kamanda wa polisi mkoa wa Tabora  afike,huku wakidai kuwa eneo hilo limekua ni tatizo sugu kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
Eneo hili linaitwa Iduguta mpakani mwa  eneo la Ziba ambalo lipo takribani kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana  saa 3 usiku.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top