Ojuku Abraham na Jelard LucasKATIKA kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya uzinzi inayomuandama, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.
“Maisha ya kimapenzi ya mzee Mandela yalikuwa ya ukakasi, kwa maana hiyo unataka tuseme kuwa kwa sababu hiyo, mzee huyu hakuwa kiongozi bora, unataka tuseme Bill Clinton wa Marekani hakuwa kiongozi bora kwa sababu tu alipata kashfa katika moja ya makorido ya Ikulu ya White House? Mimi nadhani haya mambo kama yapo au hayapo, hayahusiani na uwezo wa mtu kiuongozi, ni mambo ya chumbani yanayopaswa kuachwa huko,” alisema Lissu.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe.
Lissu alikuwa akirejea baadhi ya sababu zilizosababisha mgogoro kati
ya chama chake na Naibu Katibu Mkuu wao aliyetimuliwa, Zitto Kabwe,
anayedaiwa kushiriki kuandaa waraka wenye nia ovu, ambao pamoja na mambo
mengine, ulitaka kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu, akiwemo
Mwenyekiti wa Taifa, kwa kudaiwa kuwa na elimu ndogo pamoja na kukosa
uaminifu katika ndoa yake.Aidha, hivi karibuni wakati wa kikao kilichomalizika cha Bunge mjini Dodoma, Freeman Mbowe alidaiwa kuvuruga ziara ya mbunge mmoja mwanamke (wa viti maalum) wa chama chake aliyekuwa katika ziara ya kibunge nje ya nchi, na badala yake kumtaka kuungana sehemu alipokuwepo.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro unaokitikisa chama chao, lakini alisema hatimaye Chadema itashinda na kubakia imara na akasisitiza kuwa mwavuli wa mahakama alionao Zito ukiondoka, watamtimua. GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment