Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha Mpya wa timu ya Yanga, Hans Plujim akiwa kwenye uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kukwea pia kuwafuata wana Jangwani huko nchini Uturuki wanakoendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara. Kocha huyo aliondoka jana alasiri kwenda nchini Uturuki kujiunga na Kocha Msaidizi wa timu hiyo,Charles Boniface Mkwasa na kikosi kizima cha Yanga.Kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa miezi sita ya awali na klabu hiyo,amesema amejipanga vyema kukinoa kikosi hicho pamoja na mambo mengi mno kwa klabu hiyo,ambapo pia amesema anamjua vizuri kocha wa Simba Logarusic ambaye mwaka 2012 alimchapa kwa mabao 4-1 wakati huo Plujim akifundisha Berekum Chelsea ya Ghana na Loga akiwa Ashanti Goldb SC.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top