Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MKUU wa Wilaya ya Mvomero (DC), Antony Mtaka amezusha tafrani na kulalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT),  wilayani humo baada ya kutoa kauli kwamba wasikubali kutumika kama kondomu ama tambara la deki wakati wa chaguzi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero (DC), Antony Mtaka.
Wakizungumza na wandishi wa habari mjini hapa,  wanachama hao ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walisema mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la UWT ambacho kilifanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ofisi za CCM Dakawa wilayani humo.
Walidai kuwa kiongozi huyo alialikwa kwenye baraza hilo na baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na wajumbe,   aliwaambia maneno hayo kwa maelezo kuwa kuna wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali wilayani humo, wakati wa uchaguzi huja kujipendekeza.
Kwa kweli kauli alizotuambia mkuu wetu wa wilaya si nzuri, zimetusikitisha…kutufananisha na kondomu na tambara la deni? Ametukosea kwa kweli, sisi ni watu wazima, hakupaswa kutufananisha na vitu hivyo,alisema mmoja wa akina mama hao.
Akijibu tuhuma hizo mkuu huyo wa wilaya alikiri kutumia kauli hizo na kudai kuwa hakuwa na nia mbaya kama wao walivyofikiria isipokuwa hizo ni siasa chafu za baadhi ya wanasiaa wa Mvomero.

Mwandishi sikiliza, hizo zote ni siasa chafu za Mvomero, ni kweli nimewaambia hivyo kwa sababu tunahitaji michango ili jumuiya hiyo iendelee na kama kuna aliyeguswa awasaidie. Hebu fikiria kuna viongozi wangapi wilayani kwetu, lakini hakuna hata mmoja aliyewachangia ingawa wamewapelekea barua, ila ikifika mwakani wakati wa uchaguzi utawaona wakiwaendea, ndiyo maana nimewaambia hivyo,alisema.
Akimtetea mkuu huyo wa wilaya, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mvomero, Rachel Kingu alisema kiongozi huyo aliwaambia wanaUWT hivyo kwa sababu wilaya hiyo imekuwa na wanasiasa wenye siasa za uchochezi na kuwataka wanachama wake  kuwa makini.

Credit: GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top