Rafiki wa karibu wa familia ya Nelson Mandela, Bantu Holomisa amesema madaktari walikata tamaa kiongozi huyo na kumwondolea mashine ya kupumulia na kufariki dunia baada ya saa mbili.

“Alionekana ametulia kana kwamba amelala na hiyo
ilionyesha kuwa madaktari walikuwa wameshakata tamaa na wamefikia mwisho
wa kupigania maisha yake,” alisema Holomisa na kukaririwa na Shirika la
Habari la AP.
Rafiki huyo wa Mandela ambaye alikuwa na familia
hiyo kabla na baada ya Mandela kutoka gerezani mwaka 1990, aliiambia AP
kwamba aliitwa na wanafamilia hasa baada ya hali ya Mandela kubadilika
na kuwa mbaya zaidi.
Holomisa alisema alipofika nyumbani, alikuta
wanandugu 20 wamekusanyika wakiwa wamemzunguka. “Niliona watu wakiwa
wanahangaika naye na nilijua tu kuwa sasa imefikia hatua ya mwisho...
baada ya saa mbili, Mandela alifariki dunia.”Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment