Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye kashfa ya ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya viongozi wa CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa hiyo ilitokea mwaka 2011/12.
 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.

Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
 

Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo

Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani.

CREDIT : Mwananchi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top