Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MV Merci II ikianza kuzama majini katika gati la Kilwa Masoko.
Sehemu ya chini ya MV Merci II.…
MV Merci II ikianza kuzama majini katika gati la Kilwa Masoko.
Sehemu ya chini ya MV Merci II.
Meli hiyo ikiwa imefunikwa na maji.
MV Merci II kabla ya kuzama.
Na Abdulaziz Video, Kilwa
Meli ndogo ya mizigo ya MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro imezama katika bandari ya Kilwa masoko. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nice Mtega fundi mkuu wa meli hiyo anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo.


Akiongea na Michuzi Blog, Meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea Songosongo na  kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo nahodha wake Charles Kalinga na wasaidizi wake watatu walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliyekuwa ndani hajaonekana hadi sasa.

Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana.
(Picha na Michuzi Blog)---Via GP

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top