Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

BAADA  ya  mauaji ya Diwani wa Kata ya Kisesa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Clement Mabina (pichani) yaliyotokea Desemba 15, mwaka huu, Jiji la  Mwanza limekuwa  la moto, baadhi ya watu wana hofu, wengine kukimbia makazi yao kutokana na msako mkali wa polisi kuwanasa watuhumiwa.

 

Mwili wa Mabina baada ya kushambuliwa.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa jijini hapa, hali imekuwa tofauti  na matukio mengine kwani askari wamekuwa wengi wakihakikisha wanawanasa watuhumiwa waliohusika katika tukio hilo.

Mwanza haikaliki, kila kona askari wametapakaa na baadhi ya watu wanakimbia  mji hadi suala hili litakapopoa,” alisema mmoja wa wakazi wa jijini hapa.

Mabina ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza aliuawa na wanakijiji  baada ya kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mtoto mwenye umri wa miaka 11.

Wanakijiji  wa Kanyama walitumia silaha za jadi kumshambulia Mabina hadi alipofariki  dunia alipokuwa akipanda miti na kutengeneza njia kwa ajili ya kupitisha trekta lake kwenye ardhi  yenye mgogoro.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top