Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
            

Timu ya arsenal leo imejikuta ikipigwa kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwa timu ya manchester city katika uwanja wa etihad jioni ya leo ,

Timu ya man city ilionekana tangu mwanzo kuwa inahitaji ushindi katika mechi ya leo iliwachukua dakika 14 aguero alipoipatia timu yake goli la kwanza bada ya samir nasri kuiga kona na aguero bila ajizi akautia mpira huo nyavuni.  Dakika ya 31 THEO WALCOTT akaipatia goli la kusawazisha Arsenal lakini goli hilo lilidumu kwa dakika 8 tu msambuliaji wa man city raia wa Spain Negredo dakika 39 akaipatia city goli la pili hadi mapumzika Man city 2 Arseanl 1.
Kipidi cha pili kimeanza mnamo daika ya 50 kiungo mkambaji wa Fernandinho akaipatia man city goli la 3 na la 4 katika dakika ya 58 ya mchezo huo huku ngome ya Arsenal ikionekana imepwaya bada ya beki wake wa kutumainiwa kutoka bada ya kuumia katika dakka 42 koscielny na nafasi yake kuingia Vermaelen .
Ilikuwa ni dakika ya 63 walcott aliipatia Arsenal goli la pili goli hilo lilikaa kwa dakika 3 tu David silv akaongeza goli la 5 katika dakika 66 ,  ikiwa imebaki dakika 4 za muamuzi beki wa Arenal Per meetsacker akafunga goli la 3 ,Nae Yaya Toure alikamilisha karamu ya magoli katika dakika 90 +4 kwa mkwanju wa penaty bada ya goli kipa wa Arsenal kumuangusha mchezaji wa man city kwenye eneo la hatari. 
Man city wamebanda kwenye msimamo wa ligi kuu hadi nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal yenye point 35 na Chelsea yenye point 33 baada ya kushinda leo .

Hadi dk 90 Manchester city 6 vs Arsenal 3.
Matokeo mengine ya mechi za leo  CARDIFF 1- 0 WEST BROM,EVERTON 4-1 FULHAM,NEWCASTEL 1-1 SOUTHAMPTON, CHELSEA 2-1 C PALACE, WEST HAM 0-0 SUNDALAND


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top