Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Rose Temba, alisema ombi hilo limekosa thamani katika jicho la sheria.
Jaji
Temba alisema Oktoba mwaka huu, mawakili wa Ponda walivyowasilisha ombi
hilo kabla jalada halijapelekwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu Dar es
Salaam alipata fursa ya kulipitia na kubaini upungufu kwenye hati ya
kiapo.
“Nilishangaa
Desemba 2 mwaka huu, wakili wa Ponda, Juma Nassoro alipinga kiapo hicho
kilikuwa hakina dosari… binafsi nilipitia jalada na kuona rekodi za
mahakama haziko sahihi na zilirekebishwa kinyemela baadae, kitendo hicho
kinahesabika kama ni utovu wa nidhamu.
“Ukiukwaji
huu hauwezi kuachwa hivi hivi bali vyombo vinavyoshughulika na nidhamu
kwa mawakili nchini viwachukulie hatua mawakili wa Ponda,” alisema.
Akizungumzia
hoja ya kiapo kuwa kina dosari, Jaji Temba alisema anakubaliana na
pingamizi la awali la upande wa Jamhuri lililowasilishwa na Wakili
Kiongozi wa Serikali, Bernad Kongora kuwa kiapo hakina tarehe na baadae
kilifanyiwa marekebisho kinyemela.
“Kwa
dosari hiyo ya hati ya kiapo, mahakama inakubaliana na Wakili wa
Jamhuri, Kongola kuwa ombi la mapitio nalo limekosa thamani katika jicho
la sheria na kwa maana hiyo mahakama inakubaliana na pingamizi la awali
la upande wa Jamhuri kuwa kiapo kina upungufu,” alisema.
Desemba
2 mwaka huu, Kongora aliwasilisha pingamizi la awali akiomba mahakama
hiyo itupilie mbali ombi hilo kwa sababu hati ya kiapo ina dosari.
Oktoba
mwaka huu, Ponda aliwasilisha ombi hilo kupinga uamuzi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Morogoro kukataa kumfutia kosa la uchochezi wakati yupo
ndani ya kifungo cha mwaka mmoja nje ambacho kilimtaka asitende makosa
na awe raia mwema.
Sheikh Ponda anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti mwaka huu mkoani Morogoro.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment