WASICHANA
wawili raia wa Tanzania wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) wakihusishwa na pipi 187 za dawa za kulevya
aina ya heroin zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 135 walizokuwa
wamezimeza.
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya
nchini, Godfrey Nzowa alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa 11.45
jioni katika uwanja huo.
Alisema
watuhumiwa hao walikamatwa na kikosi kazi kinachofanya kazi katika
uwanja huo, wakiwa katika harakati za kusafiri na ndege ya Shirika la
Qatar kwenda China.
Alimtaja
mtuhumiwa wa kwanza kuwa ni Mariam Makuhani (29), mkazi wa Tabata
Kimanga aliyekuwa ametoa pipi 65 kwa njia ya haja kubwa.
Mtuhumiwa mwingine ni Hadija Shomari (30), mkazi wa Magomeni Mapipa ambaye alitoa pipi 122 kwa njia ya haja kubwa.
Nzowa
alisema kuwa wanaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa mahojiano
zaidi huku wakiendelea kuzitoa pipi hizo kwa njia hiyo ya haja kubwa.
Alisema
wanawake hao walimeza pipi hizo 187 na kila moja ina uzito wa gramu 16.
Alisema mara nyingi pipi zenye uzito wa gramu 17 humezwa na wanaume.
----habarileo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment