Migogoro ya kugombea ardhi imeendelea kusababisha vifo baada kikongwe
mwenye umri wa miaka 87 mkazi wa kijiji cha Kahanga wilayani Kahama Mkoa
wa Shinyanga kumuua kwa kumpiga risasi ya kichwa mkazi mmoja wa kijiji
hicho kutokana na ugomvi wa mashamba.

Mauaji hayo yametokea ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, kuuawa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa kugombea ardhi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala, amemtaja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kikongwe huyo kuwa ni Mihangwa Maziku (40) maarufu kwa jina la Mambe, mkazi wa Kijiji cha Kahanga na kwamba tukio hilo lilitokea Desemba 15, mwaka huu saa moja asubuhi kijijini hapo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment