KESI namba 306/13 inayomkabili Nabii na Mtume wa Kanisa la Ephata la
Dar, Josephat Mwingira, ya kuzaa na mke wa mtu, Alhamisi iliyopita
iliunguruma mahakamani naa kusababisha watu kufurika wanaoaminika kuwa ni
waumini wake.
Mtume na Nabii Josephat Mwingira.Kesi hiyo ilipoanza kuunguruma, Nabii Mwingira aliwakilishwa na Wakili Moses Kaluwa ili ikiwezekana amnasue kwenye aibu hiyo.
Hakimu Riwa baada ya kuitaja kesi hiyo aliutaka upande wa utetezi kuwasilisha utetezi wao mahakamani hapo Desemba 30 mwaka huu ambapo Januari 22 mwakani itatajwa tena.
Kesi hiyo ya aina yake, iliyohudhuriwa na umati unaoaminika ni wafuasi wake Mwingira, ilisababisha hakimu aliyekuwa akiisikiliza, kuwaamuru mawakili na wangine waliovaa makoti kuyavua kutokana na joto kali lililosababishwa na watu kufurika ndani ya mahakama.
----GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment