Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mtetema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha. 


Zamaradi Mtetema.
Akizungumza , Wolper alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.

Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
Huko nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi karibuni)  kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha yangu,” alilalama Wolper.

Baada ya Wolper kulalamika sana,  lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.

 

Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top