Mtoto awekwa kinyumba na baba yake. Tukio hilo lililobumburuka hivi karibuni limewaacha watu vinywa wazi kwa sababu mtoto huyo ana umri wa miaka minane na kwamba alianza kufanyiwa ukatili huo mwaka jana akiwa na umri wa miaka saba alipokuwa darasa la pili katika shule moja ya msingi jijini hapa (jina tunalo).
AFUMWA LAIVU!
Inadaiwa
kwamba mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Pelejai (34) ambaye
ni mfanyabiashara wa mkaa, amemwingilia mwanaye huyo kwa mwaka mmoja.
Taarifa zinasema, mwaka jana baba huyo aliwahi kufumwa laivu na mkewe akimtendea ubaya huo binti yake huyo.
Hata
hivyo, inasemekana kuwa baada ya kunaswa chumbani kwake na mtoto,
alimuomba msamaha mkewe ambaye alimsamehe kwa sharti la kutorudia tena
kufanya tendo hilo la aibu na jambo hilo likawa siri kati yao.
Akizungumza
kwa uchungu na Mdodosaji wetu katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru
anakopatiwa matibabu, mtoto huyo alisema chanzo cha baba yake kumbaka ni
baada ya mzazi huyo kugombana na mama yake ambaye aliondoka nyumbani na
kwenda kwao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
MARA YA KWANZA
Alisema mara ya kwanza kuingiliwa na baba yake alisikia maumivu makali mno huku akitokwa na damu nyingi.
Alieleza kuwa alijaribu kulia na kupiga kelele usiku huo lakini baba yake alimziba mdomo ili asitoe sauti.
Alisema
alipomaliza kumfanyia ‘unyambilisi’ huo alimtishia kuwa endapo atasema
popote, yeye atakamatwa na kufungwa na wao watabaki bila baba, hivyo
watateseka kwa njaa.
Baada
ya muda mtoto huyo alieleza kwamba baba yake huyo aliendelea
kumwingilia mara kwa mara wakati kaka yake mkubwa wanayeishi naye
akishindwa kusema baada ya kupewa fedha na baba yake.
MY GOD! KITANDA KIMOJA!
Alisimulia
zaidi mtoto huyo alisema kwamba alikuwa akilala na baba yake kitanda
kimoja kila siku kama mke na mume katika kipindi ambacho mama yake
alipokwenda kijijini kwao Nduruma wilayani Arumeru kujifungua na kukaa
kwa zaidi ya miezi mitatu.
“Ukweli nilichoka kubakwa na baba yangu lakini chanzo cha yote ni mama kutokuwepo nyumbani,” alisema mwanafunzi huyo.
Kwa
upande wake, mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa aligundua tukio la
kubakwa kwa mwanaye tangu Machi mwaka huu na baada ya tukio hilo mumewe
alimwomba tena msamaha kwa mara nyingine na yeye kumsamehe.
Mama huyo alisema kwamba alilazimika kwenda nyumbani kwao baada ya ujauzito aliokuwa nao kuwa mkubwa.
Alisema
baada ya kujifungua aliendelea kuishi huko hadi Novemba 28, mwaka huu
alipolazimika kurejea na kichanga chake baada ya kupata taarifa za
kupotea kwa mtoto wake huyo anayedaiwa kubakwa na baba yake.
Alisema
aliporejea nyumbani kwake Kambi ya Fisi alimuuliza mtoto wake mkubwa
iwapo baba yake alirudia tabia ya kumbaka mwanaye lakini mtoto huyo
hakusema chochote.
Akiwa
anatafakari sehemu alipokuwa mwanaye ndipo alipopata taarifa kwamba
alikuwa kituo cha polisi alikopelekwa na walimu wake baada ya watoto
wenzake kutoa taarifa kwa walimu kuwa mwanafunzi mwenzao amekuwa
akibakwa na baba yake mzazi.
SHULENI
Mmoja
wa walimu katika shule hiyo alithibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo
baada ya kumhoji na kumkagua na kugundua kwamba ameharibika sehemu nyeti
na kuwa kama za mtu mzima.
IGP - Said Mwema.
HOSPITALINI
Mama
wa mtoto huyo akisaidiwa na walimu walitoa taarifa kituo cha polisi na
kupatiwa hati ya matibabu (PF-3) na kumpeleka Hospitali ya Mount Meru.
Mwalimu
wa shule hiyo alisema baada ya vipimo, daktari alithibitsha kwamba
mtoto huyo alibakwa na kuharibiwa sehemu zake za siri.
Baada
ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi, vijana wa Inspekta Said
Mwema walimtia mbaroni mtuhumiwa huyo na kumfungulia kesi ya ubakaji kwa
hati ya mashtaka AR/RB/16064/2013-
UBAKAJI
Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
INAUMA SANA!
Hivi
karibuni kumeibuka vitendo vingi vya ubakaji na unyanyasaji kwa watoto,
hivyo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na
taasisi nyingine za utetezi wanaombwa kuingilia kati ili kuwanusuru
watoto na ukatili huo.
---GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment