WAKATI
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha
magazeti ya Mwananchi,Mwananspoti na The Citizen, ikikabiliwa na tishio
la wafanyakazi wake kuhamia Kampuni ya News Habari 2006, inayochapisha
Magazeti ya Mtanzania,Rai,The African na magazeti ya michezo ya Dimba na
Bingwa, Uongozi wa Kampuni hiyo unatajwa kwa kashfa nzito ya ufisadi,
baada ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa maslahi dhidi ya Waandishi
wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira,(Correspondent).
Waandishi hao wameingia kwenye mgogoro huo na Kampuni hiyo, baada ya kupewa mikataba feki ambayo walidai kuwa ni mikataba ya kifisadi,Wakizungumza na Habarimpya.com kwa nyakati tofauti, huku wakitoa masharti ya majina yao kutotajwa mtandaoni walisema kwamba, Mwananchi imekuwa ikifanya ufisadi mkubwa katika suala la maslahi ya waandishi wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira kwa kipindi kirefu
Mwandishi mwingine ambaye pia alionyesha kukerwa na kile walichokiita kuwa ni ufisadi alisema kwamba,Kampuni hiyo imekuwa ikijigamba kwamba waandishi wao hawaruhusiwi kupewa nauli ama hata bahasha za maji ya kunywa, kutoka vyanzo vyao vya Habari kama ilivyo zoeleka kwa tasnia ya habari Tanzania (Mshiko), kwa kutangza kwenye magazeti yao huku waandishi wao wasiokuwa na mikataba ya ajira, wakiendelea kufanyakazi bila kujua kiwango sahihi cha malipo ya kazi zao.
"Kila mara tunatangazwa kwenye magazeti yao, kwamba haturuhusiwi kuchukuwa bahasha yoyote kutoka kwa wadau wetu wa habari, kwa madai kwamba hiyo ni rushwa na kwamba wao hawanunui habari bali wanauza habari, lakini sisi kama waandishi tunaishi kwa shida huku watu wachache wakineemeka kupitia kazi zetu, ukianza kuhoji undani wa maslahi yako unaishia kufukuzwa kazi,pili tunafanyakazi bila mikataba yoyote na baada ya kudai hilo kwa kipindi kirefu wakaleta mkataba mpovu, ambao kama ungetolewa na taasisi nyingine, wangeandika habari katika ukurasa wa kwanza kwa maandishi makubwa ya Ufisadi wa kutisha,"alisema mwandishi huyo kwa huzuni, huku akimwomba mwandishi wa Habarimpya.com nauli ya kurudi nyumbani kwao baada ya kutoka ofisini.
Uchunguzi uliofanywa na Habarimpya.com kuhusu maslahi ya waandishi katika Kampuni hiyo unaonyesha kwamba, kati ya mwaka 2009 hadi 2013 zaidi ya waandishi 30, waliofanya kazi katika Kampuni hiyo bila kuajiriwa kati ya miaka mitatu hadi mitano, wamefukuzwa kazi baada ya kudai maslahi yao. Chat Room Baadhi ya Waandishi waliowahi kufukuzwa kazi katika kipindi hicho ni pamoja na,Mussa Mkama,Gidius Rwiza,Ummy Muya,Aziza Nangwa,Patricia Kimelemeta (huyu alifanyakazi zaidi ya miaka saba),Prisca Mussa,Nora Damian,Jesca Nangawe,Festo Polea,Frank Aman,Clara Alphonce,Icer Kimaro,Said Powa,Aziza Mosoud,Bakari Kiango na wengine wengi,wakati baadhi ya waandishi waliofukuzwa kazi ama kuacha kazi kwa majungu ni pamoja na Mwasu Sware,Joyce Mmasi (huyu baadaye aliajiriwa tena),Mwanamkasi Jumbe (baadaye alipelekwa idara ya matangazo),Mnaku Mbani,Josta Mwangulumbi,Kidanka,Sarehe Ally,Daniel Mbega na Machira.
Akizungumzia suala hilo mmoja wa Wahariri wa Habari wa Kampuni hiyo, aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema kwamba,"Kiujumla mwenendo wa Kampuni hii kwa Correspondent, si sahihi hata kidogo, kwani hata sisi ambao tuko katika ngazi ya wahariri tumesha shauri sana lakini hakuna kinachofanyika,badala yake unashangaa kuona watu wanafukuzwa kazi kila wanapodai maslahi yao, kwakweli hili si jambo zuri hata kidogo, hatuoni sababu ya kukaa na mfanyakazi kwa zaidi ya miaka mitano kwa ahadi ya kumwajiri kisha unamfukuza kazi, baadaye una ajiri watu wengine kwa mshahara makubwa hii ni kinyume hata kwa sheria za nchi, tena kwa gazeti ambalo linaongoza kwa sera ya kutetea maslahi ya watanzania wengine huku watetezi wenyewe wakinyanyaswa kiasi hiki".
Oktoba mosi mwaka huu wafanyakazi hao walipewa mikataba ya makubaliano ya kufanyakazi kwa mara ya kwanza, huku ikiwa na mapungufu lukuki na wakitakiwa kuisaini haraka ili utekelezaji wake uanze Oktoba 15 mwaka huu, moja ya mapungufu makubwa yaliyowashangaza waandishi hao ni pamoja na kiwango cha malipo ya kazi zao, ama mshahara wao kutotajwa katika mkataba huo wa makubaliano, sababu nyingine inayotajwa kwamba ni ufisadi ndani ya Kampuni hiyo ni kitendo cha mkataba huo ulioitwa wa siri kumtaka mwandishi kutojihusisha na kazi yoyote ya habari nje ya Kampuni hiyo.
Mkataba huo pia unamtaka mwandishi kutojihusisha na machapisho ya habari sehemu yoyote, ama kwa Kampuni yoyote ama kwa mtu yeyote anayefanya kazi zinazofanana na kazi za Mwananchi, wakati hawaja ajiriwa wala hawajui kiasi cha malipo yao kwa kila kazi wanazofanya, badala yake kila mwisho wa mwezi wanaambulia kati ya tsh 20,000 hadi 100,000, huku wakitakiwa kuandika habari mbili za kipekee (Exclusive Stories) kwa kila siku pamoja na makala mbili kila wiki ambazo hazijulikani kiasi cha malipo yake.
Habarimpya.com ilimtafuta Meneja Mwajiri wa Kampuni hiyo ambaye ndiye aliyesaini mikataba hiyo, Aika Masawe kupitia simu yake ya mkononi ambayo iliita bila kupokelewa
.Hivi karibuni paparazi iliandika habari juu ya kuwepo kwa mikakati ya
wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuhamia New Habari 2006, hata hivyo
aliyekuwa mhariri wa Habarimpya.com wakati ho, kabla ya kuacha kazi
aliambulia vitisho vingi kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya Mwananchi.
---Habarimpya.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment