Timu ya Arsenal na everton zimetoshana nguvu ya goli moja kwa moja kwenye mchezo wa ligi kuu ya uingereza uliomalizika hivi punde na kila timu kuambulia point moja kwenye mechi hyo ilikuwa ni timu ya Arsenal walioanza kuliona lango la everton pale mesult ozil alipomalizia pasi iliyopigwa na theo walcott kwa kichwa na kumkuta alipo na kuiweka kinywani kaika dakika ya 80 ya mchezo huo imepita dakika 4 tu mchezaji aliyetokea benchi Deulofeu aliipatia timu yake goli la kusawazisha hadi mpira unaisha ARSENAL 1 VS EVERTON 1. Kwenye mchezo huo kocha wa Arsenal alifanya mabadiliko ya kuwatoa wachezaji watatu na kuwainiza wachezaji watatu katika dakika ya 68 waliotoka ni Ramsey ,Carzla na Wilshare na nafasi zao kuchukuliwa na Flamini, Walcott na Rosicky mabadiliko hayo yalileta mafanikio katika dakia ya 80 pale walcott alipo toa pasi ya goli . dakika ya 81 kocha wa Everton alomtoa Pienaar na nafasi yake kuchukuliwa na Osman pia dakika ya 79 alimtoa Mirallas na akaingia Deolofeu ambaye ndio mfungaji wa bao la everton mnamo dakika za nyongeza everton ilimtoa Barkley ambaye kwenye mchezo huu alicheza vizuri sana na kuingia Naismith dakaka ya 90+3, wachezaji waliopata kadi za jano kwenye mchezo huu ni Barry dk 43, McCarthy dk 61, Howard dk 77 na Deulofeu dk 90+3. Arsenal imebakia kileleni kwa point 35 nyuma ya Chelsea wenye point 30 huku everton akiwa na point 28 nafasi ya 5. Mchezo uliochezwa mapema leo Fulham imeigunga Aston villa goli mbili bila kupitia kwa Delph 19 na Herd 67 ikisalia na point 13 nafasi ya 18 |
| |
|
Post a Comment
Post a Comment