Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua jana usiku jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.

Polisi imesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana jioni. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jiji la Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake hawezi kuendelea kuangalia timu yake ikifungwa kila siku kabla ya kuruka ghorofani.
 “Mashahidi wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana wa jiji la Nairobi kufahamu English Premier League ni mchezo tu kama ilivyo michezo mingine na hivyo waache kuchukua hatua za namna hii kisa michezo. Hii si mara ya kwanza kwa kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya michezo inayochezwa  England,” alisema Kibue. 
source:shaffihdauda.com

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top