Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Hivi majuzi mwanadada Huddah Monroe wa Kenya alitoa kauli kwenye mtandao kwa mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond platnumz juu ya Wema Sepetu kwa kumwambia kuwa “asihangaike na wadada wengine kwani wema ndio kipenzi chake na hao wengine wote ni wapiti njia” kauli ambayo kwa muda mfupi tuu imemfanya mwanadada huyo awe gumzo la mitandao hapa nchini na “kuchafua hali ya hewa” huko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na isiyo ya kijamii kwa watu wanopenda na wasipoenda penzi la wawili hawa

 


Uchunguzi uliofanya na bongomovies umebaini kuwa mashabiki wengi wa muziki na filamu hapa nchini wanapenda sana mahusiano baina ya wawil hawa (Wema na Diamond) kiasi cha kusababisha kuanzishwa kwa makundi mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii yakichochea wawili hawa kuoana na ikiwezekana kuzaa watoto haraka iwezekanavyo.

Katika pitapita zetu kwenye mtandao tuliweza kupata kauli hizi za watu mbalimbali wakimsifia Huddah kwa kauli yake hiyo huku wengine wakimuona kama ni shujaa….

“Umenifurahisha sana leo yaan had nime comment!!@huddahmonroe”

 mmoja wapo aliandika…


“Kuanzia leo nakupenda bureee....na nakufollow@huddahmonroe”

mwingine aliongezea…

“Nakupenda bureee Huddah we ni shujaa”… mwingine naye aliongezea huku wakidiriki kusema kuwa wawili hawa wakioana basi itakuwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa kwao.

 Bongo Kazi kweli kweli!

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top