
BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.
Akizungumza na mapaparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.
“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani.
“Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.
Paparazi wetu aliposhindwa kumpata Ray kwa kumpigia simu lilimtumia ujumbe ambapo alijibu kwa kifupi.
“Dah, kiukweli kama Nora ndiye kasema hivyo basi mimi sina comment yoyote na madai hayo na kirahisi naomba uandike hivyohivyo,” alijibu Ray.
Kwa upande wa Johari alipotumiwa ujumbe aliendelea ‘kunyuti’.
---GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment