Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PM No comments


Mwanamke ambaye ambaye hajafahamika mara moja amefariki dunia Jana jioni katika mtaa wa Posta mjini Moshi kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea baada ya kuacha njia na kumkuta mwanamke huyo.Mashuhuda waliokuwepo katika tukio hilo wamesema mwanamke huyo alikuwa ametoka katika shughuli za kibiashara katika soko lililopo mjini hapo.


Duru za habari zimeendelea kujuza kwamba mwanamke huyo ni Mnyakyusa aliyeolewa na Mchaga wote wakazi wa KCMC Mjini hapa.
imekuwepo katika tukio hilo na kushuhudia gari aina ya Fuso lililosajiliwa kwa namba T 209 AHA likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika mara moja.
Mashuhuda wanasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliosababishwa na dereva wa Fuso aliyekuwa amelewa.



Wameongeza kuwa watu wawili wamejeruhiwa kufuatia tukio hilo, ambao ni dereva wa bodaboda na rafiki yake waliokuwa wamepaki pembezoni mwa mtaa huo wakisubiri wateja.
Dereva wa Fuso hilo lililokuwa na maandishi yanayosomeka "AINULIWE BWANA" anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC na taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo zitatolewa mpaka pale upelelezi utakapokamilika.






















SOURCE::: JAIZAMALEO

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top