
Kwa jinsi inavyoonekana hapa jijini Dar-Es-Salaam, kila kukicha
foleni kama inaongezeka na imekuwa ikileta kero sana kwa wakazi wa jiji
hili ambapo mambo mengi huwa hayaendi kama inavyotakiwa kutokana na
wakazi kushindwa kufika maeneo ya mipango yao katika muda muafaka. Na
hii hali ya foleni ya jiji la Dar husababishwa na kuongezeka kwa magari
mengi na pia kuwa na barabara finyu ambapo ikitokea hali ya mvua kidogo
tu basi hali ndo inazidi kuwa mbaya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo, Mheshimiwa na
mfanyabiashara mkubwa jijini Dar Bw. Mohamed Dewji alitoa malalamiko
yake katika akaunti yake ya twitter kuwa anahitaji kuwa na Helicopter
ili aweze kuwahi na kuepuka foleni ya jiji la Dar. Na hii hapa chini
ndiyo kauli aliyotoa Mheshimiwa huyo baada ya kulazimika kupanda usafiri
aina ya Boda Boda ili asichelewe kufika katika mkutano ambao alitakiwa
kuhudhuria …

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment