![]() |
| Bob Junior na Ashley |
Ashley pia ni promota wa muziki na amekuwa akifanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika mashariki kwa kuwapeleka ujerumani kufanya shows na kwasasa yupo Kenya.
Habari ni kuwa hata ndoa ya Bob Junior imevunjika kisa kikiwa ni wawili hao kujinafasi kwa raha zao. Baada ya habari hizo kuanza kuenea na kufika hapa Swahiliworldplanet ilibidi kuwatafuta
wasanii hao wawili ili kuwauliza kuhusu issue hiyo na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Ashley ambaye alitumiwa ujumbe juzi kuhusu kuwa mapenzini na Bob Junior na alijibu kwa ufupi "sijui lolote samahani" na alipobanwa zaidi alisema "sisi sio wapenzi we are just friends ....more information muulize mwenyewe"
Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bob Junior na kumtumia ujumbe jana ila leo akajibu ujumbe huo kwa kusema "hapana si kweli, hata blog iliyotoa habari hiyo inaitwa Udaku blog so nadhani ushajua hakuna ukweli". ilipomuuliza kwa hiyo upo na mkeo
Halima(ambaye ni muigizaji wa filamu) kama zamani hamna tatizo lolote alijibu kwa kusema "kwa sasa sina mke kaka nipo single"
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment