Kiungo wa Arsenal,Jack Wilshere amesema kuwa hatopenda
kumuona mchezaji wa Manchester United,Adnan Januzaj anawekwa katika
kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza na Chama cha Soka cha nchi hiyo
FA.
Januzaj mwenye umri wa miaka 18 alijiunga na Man United mwaka 2011,anataka kupewa uraia wa Uingereza na itawezekana iwapo tu atakuwepo kwenye nchi hiyo mpaka Februari ya mwaka 2018.
Kinda huyo mzaliwa wa Belgium angeweza pia kuchagua kuzichezea timu za taifa za Serbia,Albania na Turkey ingawa ni nchi ambazo hazijapewa kibali au ruhusu rasmi na FIFA.
Wilshere alisisitiza kuwa wachezaji pekee wa kuichezea England ni waingereza na siyo watu kutoka mahala pengine.Huku akisema kuwa kukaa Uingereza kwa zaidi ya miaka mitano haimaanishi wewe ni Muingereza.
Pia aliendelea kusema kuwa kama yeye akienda Uhispania na kukaa kwa miaka mitano haimaanishi aichezee timu ya Taifa hilo.Na akaongeza kuwa sifa ya waingereza ni kukaba kwa nguvu na kujituma sana uwanjani ni asili yao hivyo ni tofauti kabisa na mataifa mengine.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment