Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kiasi cha Waislamu milioni mbili kutoka karibu mataifa yote duniani walikusanyika katika mlima Arafat nchini Saudi Arabia hapo jana, wakijiunga pamoja katika imani yao ya haja ya kuitakasa kiroho mwanzoni mwa hija ambayo hujafanyika kila mwaka. Katika eneo hilo la mlima Arafat, ambako kuna nguzo zinazoashiria mahali pa mlima wa toba, unaotambulika kwa lugha ya Kiarabu kama Jabal al-Rahma. Ni muda muhimu katika ibada ya Hija wakati waumini wakiwa katika mlima Arafat wanaamini kuwa milango ya pepondi inafunguliwa kwa maombi kujibiwa na dhambi zilizofanywa hapo kabla kusamehewa. Mtume Muhamad S.A.W anaaminika kutoa risala yake ya mwisho katika mlima huo kwa mamia ya maelfu ya waumini akiwataka waislamu kuwa na umoja. Leo ikiwemo mataifa ya Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia wanasherekea Siku Kuu ya Eid El Haji .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top