Bety Kangonga analiripotia Gazeti la TanzaniaDaima kuwa
jeshi la Polisi nchini lilimshikilia kwa muda kisha kumwachia mwanamke
mmoja anayedhaniwa kuwa ni Samantha Lewthwaite ‘Mjane Mweupe’ anayesakwa
kwa udi na uvumba kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kuhusika na mipango na
kutimiza shambulio la kigaidi lililotokea katika jengo la kibiashara la
Westgate jijini Nairobi adhuhuri ya Jumamosi, Septemba 21, 2013.
Gazeti hilo linasema lilizungumza jana kwa njia ya simu, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Suleiman Kova, ambaye alithibitisha taarifa hizo lakini akasema baada ya kufanya uchunguzi

waligundua
mwanamke huyo si mhusika wa matukio hayo ya ugaidi bali ni mke wa mtu
anayeishi jijini Dar es Salaam kisha akalitaka gazeti hili kuwasiliana
na msemaji wa jeshi hilo Makao Makuu, Advera Senso.
Kauli ya Senso: “Hapa hakuna stori, ni mwamko walionao wananchi na walifikisha kwa jeshi hili nasi tulifuatilia na baada ya uchunguzi tulibaini hakuwa mhusika…kama unavyopewa taarifa za nyumba fulani kuwa wanauza bangi, lakini ukienda na kufanya upekuzi hakuna hicho kitu, basi tunakuwa tumejiridhisha, ndivyo ilivyokuwa katika suala hilo,” alisema.
Inaarifiwa kuwa mwanamke huyo alisadikiwa kuwa ni mtuhumiwa wa ugaidi baada ya kwenda katika Benki ya Exim na kutaka kufungua akaunti pamoja na kuomba zabuni ya kufanya usafi katika jengo la benki hiyo lililopo jirani na Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Mmoja wa mameneja wa benki hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alikiri kuwapo kwa tukio hilo, ingawa hakuwa tayari kutoa taarifa za ndani, kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi wakati tukio hilo likitokea.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, waliozungumza na Tanzania Daima walisema mwanamke huyo alifika katika benki hiyo juzi akiomba zabuni ya kufanya usafi kupitia kampuni yake inayojulikana kwa jina la Osson Breeze.
Walisema hata hivyo baadhi ya watendaji wa benki hiyo waliingiwa shaka na mwanamke huyo kutokana na kufanana na mtuhumiwa huyo wa ugaidi na kutoa taarifa polisi.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment